Eric Ogenga ameapishwa kuwa karani wa bunge la kaunti ya Siaya

  • | Citizen TV
    204 views

    Hatimaye Eric Ogenga ameapishwa kuwa karani wa Bunge la kaunti ya Siaya baada ya kuwapiku wengine 11 waliohojiwa siku ya Ijumaa na Bodi ya ajira wa umma ya kaunti hiyo. Bunge la Siaya limemuidhinisha Ogenga huku wawakilishi wadi wakimsifia kuwa kuwa mwadilifu na anayeelewa vema shughuli za Bunge zinavyoendeshwa. Ogenga alikuwa kaimu karani wa Bunge Hilo kwa miaka mitano.