- 4,111 viewsDuration: 1:25Mbunge wa Kabuchai, Majimbo Kalasinga, ameitaka idara ya usalama kuingilia kati na kuchunguza tukio ambapo Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, anadaiwa kutishia maisha yake kabla ya uchaguzi mdogo wa wadi ya Chwele Kabuchai ambao umepangwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu. Akizungumza na wanahabari nyumbani kwake eneo la Sikusi, Mbunge huyo wa chama cha Ford Kenya, ambaye kwa sasa uhusiano wake na kiongozi wake wa chama umesambaratika, amesema kuwa maisha yako hatarini, akimwomba Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, kukusanya na kuchambua video za vitisho hivyo kwa ajili ya kulinda maisha yake.