- 275 viewsDuration: 3:16Walimu 25 wa shule za sekondari msingi (JSS) kutoka kaunti tisa zilizoorodheshwa kuwa na visa vingi vya ndoa za mapema na ukeketaji wamepewa mafunzo maalum ili kuwa mabalozi wa kupinga mila na desturi zinazowanyima wasichana fursa ya kuendelea na masomo.Katika warsha iliyoandaliwa mjini Nanyuki na shirika lisilo la serikali la Northern Rangelands Trust (NRT), walimu hao wamesema wasichana kutoka jamii za wafugaji bado wanakumbana na changamoto nyingi zinazozuia maendeleo yao kimasomo na kijamii.