Harambee Junior Starlets kuchuana na Burundi hapo kesho jijini Addis Ababa

  • | Citizen TV
    303 views

    Timu ya taifa ya wasichana wasiozidi miaka 17 Harambee Junior Starlets iliwasili nchini Ethiopia tayari kupambana na Burundi hapo kesho. Mechi hiyo ya raundi ya nne na mwisho kuelekea kombe la dunia inatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu huku wasichana hao wakiahidi kuweka historia kuwa timu ya kwanza Kenya kushiriki kombe la dunia. Baada ya mkondo huo wa kwanza watarudiana tena wikendi ijayo humu nchini ambapo mshindi wa jumla atafuzu kuingia kombe la dunia litakaloandaliwa nchini Dominika.