Miti ya matumaini Mandera

  • | Citizen TV
    1,289 views

    Mradi wa upanzi wa miti ulioanzishwa na serikali ya kaunti ya Mandera takriban miaka minane iliyopita, umebadilisha mandhari ya eneo hilo mbali na kuwapa ajira zaidi ya kina mama 1000. Mradi huo umewasaidia kina mama hao kupata mshahara na pia kuweza kukimu mahitaji ya familia zao. Na kama anavyotuarifu Jamila Mohamed, mradi huo umechaguliwa kwenye tuzo za shindano la kimataifa la World Green City litakaloandaliwa mwezi Septemba nchini Uholanzi.