Wanafunzi watano wanawakilisha Kenya kwenye shindano la kimataifa la hisabati

  • | KBC Video
    16 views

    Wanafunzi watano kutoka shule za humu nchini wanawakilisha Kenya kwenye makala ya 65 ya shindano la kimataifa la hisabati al-maarufu Mathematical Olympiad-IMO ambalo hufanyika kwa awamu kila mwaka katika nchi tofauti.Wanafunzi hao Cynthia Kathomi Mworia, Master Gilbert Ongoro, Tony Rotich Odhiambo, Alfred Githui Muriu na Lenny Muriungi Mutuma wanatoka shule za upili humu nchini. Shindano hili limeandaliwa katika chuo kikuu cha Bath nchini Uingereza na litafikia tamati tarehe-22 mwezi huu. Naibu mshirikishi wa kitengo cha sayansi, teknolojia ya uhandisi na hisabati katika kituo cha masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia barani Afrika-CEMASTEA, Martin Mungai ameelezea imani yake kuwa wanafunzi hao watapeperusha bendera ya Kenya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive