Moto, milipuko yamulika angani kaskazini Israel Hezbollah iliposhambulia
Majeshi ya Israeli yamefanya mashambulizi ya angani Jumatano kusini mwa Lebanon katika mashambulizi ya hivi karibuni yanayolenga wanamgambo wa Hezbollah wakati kikundi cha Hezbollah cha Lebanon kilipoishambulia Julai 15 kwa makombora ambayo mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel iliyatungua katika mji wa Kiryat Shmona.
Jeshi la Israel lilisema mashambulizi yake yalilenga miundombinu ya Hezbollah, na kwamba majeshi ya Israeli pia yalitumia makombora kujibu vitisho vya Hezbollah katika eneo hilo.
Hezbollah ilifyatua makombora kuelekea Israel, huku jeshi la Israeli likisema limezuia baadhi ya makombora hayo wakati mengine yalianguka katika eneo la wazi bila ya kuleta uharibifu au vifo.
Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah alisema wakati akitoa hotuba Jumatano kuwa kikundi cha wanamgambo hao watalenga maeneo mapya ndani ya Israel iwapo majeshi ya Israeli yataendelea kuua raia.
Shambulizi lililofanywa na Israeli Jumanne liliuua raia watano wa Syria huko kusini mwa Lebanon.
Mapigano ya mpakani kati ya Israel na Hezbollah yameongeza wasiwasi kuhusu mgogoro mkubwa zaidi kuzuka katika kanda hiyo huku majeshi ya Israeli yakiwa pia yanapigana na Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant walijadili mapigano yanayo endelea kati ya Israel na Hezbollah wakati wa mazungumzo waliofanya kwa njia ya simu Jumanne, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilieleza.
Msemaji wa Pentagon Major General Pat Ryder alisema katika taarifa yake kuwa mawaziri hao wa ulinzi pia walizungumzia kuhusu kivuko cha muda kilichojengwa na Marekani katika pwani ya Gaza ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa Palestina. -AFP, Reuters
#Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #hospitali #nasserhospital #lebanon #hezbollah #wanamgambo
13 May 2025
- This is not the first time a petition is being filed against the DCJ.
13 May 2025
- Kimani Ichung'wah, who has been receiving criticism from Kenyans, has asked for forgiveness.
13 May 2025
- The latest report highlights a paradigm shift from the traditional income-generating investments to value-driven luxuries.
14 May 2025
- The report highlights how employers subjected the women to extreme exploitation in private homes, often fuelled by racism.
14 May 2025
- The audit found that ministries, departments and agencies failed to provide documentation for Sh783.9 million in spending.
14 May 2025
- Presidential aspirants are focusing on the youth, as the 2027 general election battle shapes up.
14 May 2025
- NLC boss admitted that while the commission can investigate land grabs, it lacks authority to revoke illegal titles.
14 May 2025
- The commission said they need Sh3 billion to hire the interns on permanent and pensionable terms.
14 May 2025
- The government last week unveiled its leasing programme, handing over four public sugar factories to private players.
14 May 2025
- Chairman Anangwe says the varsity should be allowed to function without threats.
14 May 2025
- Safaricom CEO Peter Ndegwa has addressed concerns about the company's involvement in the Social Health Authority (SHA) system, clarifying that its role is limited to the digitisation of the process.
14 May 2025
- Sean "Diddy" Combs' former girlfriend, Casandra Ventura, the star prosecution witness at the hip-hop mogul's sex trafficking trial, testified on Tuesday that her music career began to suffer as she increasingly spent her time participating in days of…
14 May 2025
- Senators yesterday put Kericho Governor Dr Eric Mutai on the spot over stalled Early Childhood Development and Education (ECDE) classroom projects, some of which have remained incomplete since the onset of devolution. This even as the lawmakers…