- 69 viewsMeya wa Paris, Anne Hidalgo, aliogelea katika maji yenye matope ya Seine Jumatano kuonyesha kuwa mto huo hivi sasa ni msafi kabisa kwa ajili ya matukio ya kuogelea wakati wa michezo ya Olimpiki. Akiwa amevaa miwani maalum ya kuogelea na nguo za kuogelea, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 aliogelea kifudifudi kabla ya kuuzamisha uso wake na kutambaa ndani ya maji, akikamilisha takriban mita 100 kwenda na kurudi katika mto huo. Alikuwa ameogelea akiwa na maafisa wa ngazi ya juu na Tony Estanguet, mshindi wa medali ya dhahabu mara tatu katika mashindano ya kuendesha mtumbwi, anayeongoza kamati ya maandalizi ya Michezo ya Paris, itakayo funguliwa wiki ijayo Julai 26. “Leo ni uthibitisho kuwa tuko pale ambako tulitarajia kuwa,” Estanguet alisema. “Hivi sasa tuko tayari kuandaa michezo hiyo huko Seine.” Licha ya uwekezaji wa euro bilioni 1.4 ($1.5 bilioni) kuzuia maji taka kuvuja na kuingia katika mto huo, wasiwasi kuhusu mto huo umeenea katika jimbo la Seine kuelekea Michezo ya Paris. Lakini kuanzia mwezi Julai, kutokana na mvua kubwa hatimaye kumekuwa na hali ya hewa ya joto, sampuli zikionyesha mto huo uko tayari kwa ajili ya uogeleaji na mashindano ya Olimpiki. #meya #paris #olimpiki #mto #annehidalgo #voa #michezo #kuogelea #ufaransa #voaswahili
Meya wa Paris aogelea mto Seine kuthibitisha unafaa kutumika kwa Olimpiki
- - Duniani Leo ››
- - Kenya-Finland Ties ››
- 14 May 2025 - Presidential aspirants are focusing on the youth, as the 2027 general election battle shapes up.
- 14 May 2025 - The government last week unveiled its leasing programme, handing over four public sugar factories to private players.
- 14 May 2025 - The report highlights how employers subjected the women to extreme exploitation in private homes, often fuelled by racism.
- 14 May 2025 - NLC boss admitted that while the commission can investigate land grabs, it lacks authority to revoke illegal titles.
- 14 May 2025 - Chairman Anangwe says the varsity should be allowed to function without threats.
- 14 May 2025 - The audit found that ministries, departments and agencies failed to provide documentation for Sh783.9 million in spending.
- 14 May 2025 - The commission said they need Sh3 billion to hire the interns on permanent and pensionable terms.
- 14 May 2025 - Safaricom CEO Peter Ndegwa has addressed concerns about the company's involvement in the Social Health Authority (SHA) system, clarifying that its role is limited to the digitisation of the process.
- 14 May 2025 - Sean "Diddy" Combs' former girlfriend, Casandra Ventura, the star prosecution witness at the hip-hop mogul's sex trafficking trial, testified on Tuesday that her music career began to suffer as she increasingly spent her time participating in days of…
- 14 May 2025 - Senators yesterday put Kericho Governor Dr Eric Mutai on the spot over stalled Early Childhood Development and Education (ECDE) classroom projects, some of which have remained incomplete since the onset of devolution. This even as the lawmakers…