Wizara ya leba yaweka mikakati ili kukabiliana na visa vya ulanguzi wa binadamu hasa watoto

  • | K24 Video
    25 views

    Wizara ya leba kupitia idara yake ya ulinzi wa jamii imeweka mikakati ili kukabiliana na visa vya ulanguzi wa binadamu hasa ulanguzi wa watoto ambao wanaonekana kulengwa zaidi katika biashara hiyo haramu. Hii ni baada ya ripoti ya taasisi ya kitaifa ya utafiti kuhusu uhalifu nchini NCRC kubaini kuwa watu wanne kati ya kumi wanaohusika katika visa vya ulanguzi, wawili huwa ni watoto wadogo.