Maafisa wa polisi nchini wanatazamiwa kupokea nyongeza ya mishahara kuanzia Julai

  • | K24 Video
    42 views

    Maafisa wa polisi nchini wanatazamiwa kupokea nyongeza ya mishahara kuanzia Julai mosi mwaka huu kuashiria hatua muhimu ya kuimarisha ustawi wa maafisa wa usalama. Mpango huu ni sehemu ya ajenda kubwa ya mageuzi yanayotokana na mapendekezo ya jopokazi la kitaifa la maboresho ya ustawi wa polisi lililo na jukumu la kutathmini na kuboresha mazingira ya kazi kwa mashirika ya usalama nchini.