Ikiwa ni 'Ruto Must Go' Niembieni jinsi mnavyotaka niende '

  • | BBC Swahili
    2,532 views
    Rais wa Kenya William Ruto amepuzilia mbali wito ambao umekuwa ukitolewa na waandamanaji na viongozi wa upinzani kumtaka ajiuzulu, na kuwapa changamoto kutoa mpango mbadala ufaao badala ya kuchochea ghasia na machafuko nchini. Akizungumza huku kukiwa na ongezeko la mvutano wa kisiasa na maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali yake, Rais Ruto alipuuzilia mbali wito "Ruto lazima aondoke", ambao pia umekuwa ukitolewa kwenye mitandao ya kijamii na kusema hayo ni maneno yasiyo na msingi. Aidha amesema wanaomtaka aondoke wanafaa kutoa mpango wa jinsi atakavyoondoka madarakani . Je matamshi haya yana maanisha nini? @RoncliffeOdit anachambua kwa kina suala hili na mengine mengi leo usiku katika Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #kenya #diratv Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw