Viongozi wa kidini wapongeza kusitishwa kwa maandamano

  • | Citizen TV
    278 views

    Baadhi ya viongozi wa kidini kutoka kaunti ya kakamega wamepongeza hatua ya vijana kusitisha maaandamano ya kushinikiza mabadiliko serikalini. Wakizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kanisa katika Kijiji cha eshiandukusi eneo bunge la lurambi, makasisi hao pia wamewataka wabunge kutumia mamlaka yao ya kutunga sheria kuangazia mahitaji ya wananchi wala sio kutetea maswala yao binafsi