Wakulima wa vipepeo eneo la Gede kaunti ya Kilifi waandamana kupinga uongozi mbaya

  • | Citizen TV
    359 views

    Wakulima wa vipepeo eneo la Gede kaunti ya Kilifi wameandamana wakilalamikia kile walichokitaja kama uongozi mbaya katika mradi huo wa Vipepeo ndani ya makavazi ya kitaifa ya Gede. Wanadai kuwa usimamizi wa sasa katika makavazi hayo umekuwa ukiwanyanyasa licha ya wao kujitahidi kuimarisha mradi huo.