Jamii mipakani zahimizwa kudumisha amani

  • | KBC Video
    52 views

    Ujumbe wa amani kutoka nchi jirani ya Somali, viongozi na baraza la wazee wa kaunti ya Mandera wanawahimiza wakazi wa eneo la kaskazini mwa Kenya kuimarisha amani miongoni mwa jamii zinazoishi karibu na mipaka ya Ethiopia na Somalia kwa manufaa ya raia wa mataifa hayo matatu. Wakiongea jijini Nairobi wakati wa maadhimisho ya siku ya amani ulimwenguni, viongozi hao waliwahimiza raia wa maeneo husika kushirikiana na maafisa wa usalama ili kuwawezesha kukabiliana na visa vya mashambulizi na uhalifu ambavyo vimeshuhudiwa katika eneo hili katika siku za hivi majuzi. Wito huo umetolewa majuma mawili baada ya watu wanane kuuawa katika eneo la Banisa, kaunti ya Mandera karibu na mpaka kati ya Kenya na Ethiopia.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive