
29,126 views
20 Jun 2019
wimbo wa upendo wa Mungu #StPaulsStudentsChoir #vol8 #SautiTamu Pendo la Marafiki ni mojawapo ya nyimbo katika kanda ya nane (vol 8) St. Paul's Students Choir, Chuo Kikuu cha Nairobi, Kinanda kimechezwa na Mkude Sekulu Wimbo umetungwa na kutayarisha na Martin Munywoki Tazama kazi nyingine za kwaya katika channel hii na ile ya kwaya, kama vile Msisimko wa Sifa, Nitakutukuza Mungu, Mwangaza, Natazama Kalvari, Asifiwe Bwana Mungu, Chagueni Mtakayemtumikia, Mmepewa Bure, Misa Upendo, Umenifilia Mimi n,k MANENO YA WIMBO Ninyi ndinyi mmenikamilisha kamilisha (hadi) Hadi nikawa hi-vi mi-mi nilivyo (ndugu zangu) Ni Mungu Baba ndiye aliyetukutanisha (japo) Japo hatulingani tumekamilishana {Katika pendo lenu - ndipo nimeelewa jinsi Mungu alivyo Nimemuona - Mungu macho kwa macho } *2 Nikiwa na njaa - Ni ninyi marafiki zangu mnimegeao mkate Penye machungu na maumivu makali - Ni ninyi marafiki zangu mwaniuguza majeraha Nikitawaliwa na hofu - Ni ninyi marafiki zangu mnaonipa moyo upya Tena nikipotea njia - Ni ninyi marafiki zangu mwanirudi mwanikosoa 1. Ona tunavyosaidiana hima, wenyewe kwa wenyewe, Wakati wa furaha hata wa shida Tumeweka mbali tofauti kidaraja na mali Bahati iliyoje kuwa pamoja 2. Ona chuki, wivu, fitina, umimi, havimo kati yetu Wakati wa furaha hata wa shida Tumeweka msingi imara usiotikisika Bahati iliyoje kuwa pamoja { Pendo pendo pendo pendo - pendo letu lidumu milele Tuombeane tusaidianeni - waone Mungu kati yetu } *2 Wasitenganishwe - wapendanao Waombeeni - baraka tele sitenganishwe - wapendanao Waombeeni - baraka tele, pendo na lidumu unaweza kuutumia kama wimbo wa sherehe za harusi/ndoa au za shukrani. nyimbo nyingine za harusi ni kama kipenzi changu, pokea pete, nimekuchagua wewe, mpendwa wangu, nakupenda, n.k
