
3,299 views
Watunza Misingi feat Gome Jero, Makanta and Oby Hard
23 Jan 2022
#WATUNZAMISINGI #TUNATENDA ALBUM: Si.Be SONG: TUNATENDA GEN's:GOME JERO,MAJANTA, & OBY HARD SILAHA BEGANI (Si.Be) NI ALBUM YA PILI TOKA KWA WATUNZA MISINGI. ALBUM HII RASMI ITAACHIWA TAR 29.01.2022 TUNATENDA NI NGOMA YA PILI KUACHIWA TOKA KWENYE ALBUM HII TEMBELEA KURASA ZETU KWA KUJIUNGA NA SISI KATIKA SAFARI YA KUJIFUNZA KUPAMBANA ILI KUKOMBOKA KIFIKRA,KIUCHUMI na KIUTAMADUNI VERSE GOME JERO Tunagangamara kwa lolote Na kwa fikra zote vyovyote Tunahima imara hii popote Tayari kwa lolote Habari kwa yeyote Pema petu wote, chema chetu sote Kibaya tusiokote,baya si lolote Ujokeri uteja starehe za shaka Ubepari ubeberu usikubebe ni matata Uhuni umalaya na fani usibake Fanani kukataa katakata usichoke Utamaduni duni kudumishwa usitake Kukurupushwa na maisha kurushwa Kwa hatua kutua usipojua tambua Si mahala pake si fumbo fumbua Si fimbo tatizo tatua Lipizo usilipize maana yake Makosa tunakosa sisi sote siku zote Tutubu tutubuni tusitemane mate Na tena tenda tunatenda ubunifu usitutoke Ufaham akili timam mara dufu Tunatenda uaminifu CHORUS: GOME JERO TUNATOA MASHAKA NA HOFU MATATA NA UTOVU WA NIDHAM TUNATENDA MATENDO KWA MWENDO WA FASIHI SIMULIZI NA ANDISHI TUNATOA MASHAKA NA HOFU MATATA NA UTOVU WA NIDHAM TUNATENDA MATENDO KWA MWENENDO WA FASIHI SIMULIZI NA ANDISHI TUNATENDA HURU TUNATENDA UHURU EEEH! VERSE 2:MAJANTA Yooo! Chini Kwa chini,we are not televised/ Pima darubini,future yetu na vizazi/ Alkebulan,Dunia nzima mpaka Mars/ Iko wazi,ma element keeper,ma teacher na ma preacher/ Ma brake dancer, graffiti kwenye ukuta/ We surround the enemy,from the scratch/ Ma path finder,beat cruiser,juu ya land nakimbiza/ Huru kama cypher,vyenye tuko na machata na yatunza mpaka kufa/ Tulia uliza,beti zinawafunza/ Sisi kama sisi, clockwise tunatanda/ Against uduanzi tuko serious,miaka Rudi miaka nenda/ Ma jenerali,vikosi vya Askari wenye Mori/ Infantry soldiers tunapiga doria/ Tulizaliwa kuwa tuna thubutu na kutenda independtly/ kufa mara moja no retreat no surrender/ Hautaki nenda,tunafanya tunacho penda/ Move bila uoga wakulungwa hata wakisema tumepinda, Tamaa tushaishinda/ Mavumba msamiati katikati ya harakati/ Mwendo wa jet,huwaga hatubadiliki itikadi hadi tamati/ Iwe wanataka au hawataki/ Tumeamua kusadiki usawa halisi/ Tutabaki kuwa sisi visima Oasis/ Waandishi wamiliki,makomredi wa ku attack/ Moko moko front,we shall never turn back yoo/ Na si udanganyifu uarifu arifu Tunatoa mashaka na hofu Matata na utovu wa nidham Tunatenda matendo kwa mwendo Wa haki harakati na upendo Tunatenda vitendo kwa mwenendo Wa fasihi simulizi na andishi Tunaishi na ngum hatudum na nyepesi Huru tunatenda uhuru
