
4,863 views
15 May 2024
NEEMA YA GOLGOTHA lyrics Nilipofika Golgotha Nikaiona huko, Neema kubwa kama mto Neema ya ajabu. Chorus Neema ya Golgotha Ni kama bahari kubwa, Neema tele na ya milele Neema ya kutosha. Nilipofika moyo wangu Ulilemewa sana, Sikufahamu bado vema Neema yake kubwa. Nilipoona kwamba Yesu alichukua dhambi, Neema ikadhihirika Na moyo ukapona. Mbinguni nitakapofika Furaha itakuwa, Kuimba juu ya neema Milele na milele. #hymn #nyimbozawokovu #neemayagolgotha #viral #trending