
6,260 views
17 Jul 2023
YESU UNIPENDAYE [1] Yesu unipendaye kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye mwovu akinijia. Yafiche ubavuni mwako maisha yangu; Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu. [2] Ngome nyingine sina; nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako, Ninakuamania, kuniweshesha; Shari wanikingia, vitani wanitosha. [3] Nakutaka mpaji, vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, utanijazi vyako; Nao waangukao wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, uongoze vipofu. [4] Bwana umeniosha moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha yapatikana kwako; Kwako Bwana naona kisima cha uzima; Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.