
2,871 views
12 Jul 2023
YESU, NAKUPENDA [1] Yesu nakupenda, u mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu: Na mwokozi aliyeniokoa Sasa nakupenda, kuzidi pia. [2] Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia. [3] Ulipoangikwa msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. [4] Mawanda mazuri na masikani Niyatzamapo huko mbinguni, `Tasema na taji nitakayovaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.