Abiria Titan asimulia kukatika kwa mawasiliano

  • | BBC Swahili
    1,095 views
    Abiria wa zamani wa chombo cha Titan aelezea changamoto ya kukatika kwa mawasiliano aliyowahi kukutana nayo mwaka 2022 alipokuwa akienda kuangalia mabaki ya meli ya Titanic chini ya bahari. Mwigizaji wa Mexico na mtengeneza maudhui wa Youtube Alan Estrada alikuwa kwenye chombo cha Titan mwaka jana kilipopoteza mawasiliano wakiwa kina cha karibu mita 1,000, na kusababisha kutaka kukatisha safari hiyo. Estrada alirekodi msafara huo na kuliambia shirika la habari la Reuters kuwa baadaye mawasiliano yalirejea na chombo kiliweza kuendelea na safari #bbcswahili #titanic #titan