Afisa wa polisi aliyejeruhiwa na waandamanaji mjini Kisumu ameaga dunia

  • | K24 Video
    456 views

    Afisa mmoja wa polisi aliyejeruhiwa kifuani kwa jiwe lililokuwa limerushwa na waandamanaji mjini Kisumu ameaga dunia. Ben Oduor aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Nyamira amefariki mapema leo alipokuwa akitibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Aga Khan. Wakati huohuo baadhi ya wafanyibiashara Kisumu na Nairobi, wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya mali zao kuporwa wakati wa maandamano.