Skip to main content
Skip to main content

Afueni baada ya mwili wa Maureen uliokuwa ukizuiliwa kutokana na deni kuachiliwa

  • | KBC Video
    366 views
    Duration: 2:02
    Ni afueni kwa Familia na wakazi wa Gachie, baada ya kuupata kwa mwili wa jamaa yao Maureen Wambui Munga, uliokuwa umezuiliwa kutokana na bili ya hospitali ili kuuzika. Maureen Wambui Munga, aliyefariki tarehe 27 mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu , mwili wake ulizuiliwa katika chumba cha kuhifadhii mwili cha Kenyatta Memorial, kutokana na bili ya hospitali ya milioni tano, katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya chuo kikuu cha Kenyatta. Licha kuchangisha shilingi 600,000 na pia kupewa msamaha wa shilingi 700,000 kupitia bima ya afya ya SHA, Salio la Sh3.7 milioni lilibaki kulipwa, jambo lililochelewesha mipango ya mazishi. Mzozo huo ulitatuliwa baada ya wakili Ivy Kinuthia kuwasilisha kesi mahakamani, ambapo Jaji Stella Mutuku aliamuru mwili huo uachiliwe baada ya kulipa gharama za chumba cha kuhifadhia maiti. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive