- 1,090 viewsDuration: 4:35Pindi tu walipotwika majukumu ya uongozi mwaka wa 2022, serikali ya Kenya kwanza ilianza upesi kutekeleza ahadi yake ya kuimarisha teknolojia nchini na kuimarisha ajira kwa vijana kupitia mitandao. Mojawapo ya miradi ilikuwa kutoa intaneti ya bure kwenye maeneo 25,000 ya umma ikiwawemo masoko. Miaka mitatu baadaye, ni vituo 2,000 pekee vya umma vimewekwa intaneti hiyo ya bure. Baadhi ya maeneo ya wachuuzi yamesalia na lalama kuwa intaneti hiyo ya bure iliacha kufanya kazi.