Aliyekua mwalimu na mwanzilishi wa kwaya ya mwakigwena Enock Ondego aaga dunia

  • | Citizen TV
    369 views

    Familia ya aliyekua mwalimu na mwanzilishi wa kwaya ya mwakigwena Enock Ondego inaomboleza kifo chake . Licha ya ondego kutunga nyimbo za kizalendo zilizotumbuiza rais wa kwanza wa kenya mzee Jomo Kenyatta, Ondego aliishi maisha ya uchochole. Kwa sasa mwili wa marehemu ungali kwenye makafani ya hospitali kuu ya pwani jijini mombasa familia ikisema ondego hakupata heshima inayositahili akiwa hai.