Aliyekuwa jaji mkuu David Maraga ataka naibu mkuu wa polisi aondolewe

  • | Citizen TV
    6,510 views

    Aliyekuwa jaji mkuu David Maraga sasa anataka naibu inspekta jenerali wa polisi eliud lagat aondolewe mamlakani ili uchunguzi wa mauaji ya mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang' uweze kufanikishwa. Maraga anatoa wito wa kukamatwa mara moja kwa Lagat, akidai kuwa ushahidi uliopo unamhusisha na mauaji ya Ojwang’. Aidha, anataka wakenya wajitokeze na kushinikiza haki kwa marehemu Ojwang' kwenye maandamano ya jumanne ijayo wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano ya Gen Z.