Aliyekuwa mkuu wa polisi Kamukunji atoa ushahidi kuhusu kifo cha Rex Masai

  • | Citizen TV
    1,579 views

    Afisa wa polisi aliyesimamia kituo cha polisi cha Kamukunji wakati wa maandamano ya Gen Z Robert Mugo amekanusha kuhusika kwa maafisa waliokuwa chini yake kutekeleza mauaji yoyote wakati wa maandamano ya mwaka jana. Mugo ambaye ametoa ushahidi kwenye uchunguzi wa mauaji ya Rex Masai, ameiambia mahakama kuwa maafisa wake hawakubeba bunduki, ila marungu na gesi ya kutoa machozi.