Askofu Kivuva apinga hatua ya Vatican ya kuwaidhinisha makasisi kuwapa baraka wapenzi wa jinsia moja

  • | K24 Video
    67 views

    Askofu mkuu wa kanisa katoliki katika dayosisi ya Mombasa ,Martin Kivuva amepinga hatua ya Vatican ya kuwaidhinisha makasisi kuwapa baraka wapenzi wa jinsia moja. kivuva ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la maskofu wakatholiki nchini amesema katu kanisa katoliki halitafungisha ndoa za watu wa jinsia moja. Hii ni baada ya Askofu mkuu wa Nairobi Philip Anyolo kutoa kauli sawia hapo jana akisema kuwa kubariki miungano ya watu wa jinsia moja hakuambatani na mafundisho ya kanisa.