Askofu wa Kanisa Katoliki akataa zawadi ya Waheshimiwa Kirinyaga

  • | Citizen TV
    5,338 views

    Wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Kirinyaga walilazimika kuelekeza kwingineko zaidi ya shilingi elfu hamsini walizokuwa wametoa kumtunuku Askofu wa kanisa katoliki Dayosisi ya Murang’a Maria Wainaina baada ya kuongoza hafla ya kutoa shukrani. Askofu huyo alikataa pesa hizo na zawadi ya mbuzi na kuwaagiza wawakilishi wadi hao kuzitoa kwa shule ya watoto wasio na uwezo wa kusikiaeneo la Kerugoya.