- 4,486 viewsDuration: 2:51Kufuatia shambulio lililosababisha watu 6 kuuawa huko kainuk, katika mpaka wa kaunti za Turkana na West Pokot, Shambulio jingine tena limeripotiwa huko Turkana, wakati ambapo waziri wa usalama Kipchumba Murkomen alikuwa ziarani kutathmini hali. Murkomen amesema kuwa serikali amewatambua wanaoeneza uhasama mpakani na mpango wa kuwapokonya silaha unaimarishwa. Aidha Murkomen amesema kuwa operesheni maalum inayolenga mpaka wa West Pokot na Turkana itafanyika katika wiki chache zijazo ili kurejesha amani.