Baadhi ya vijana Migori wataka Mswada wa Fedha wa 2024 kutoishinishwa

  • | Citizen TV
    76 views

    Baadhi ya vijana katika kaunti ya Migori wamewarai wabunge kuangusha mswada wa fedha 2024 kwani utaongeza gharama ya maisha maradufu. Wakizungumza katika kaunti ndogo ya Awendo, vijana hao walielezea masaibu ambayo wananchi watapitia pindi tu Mswada huo utakapo halalishwa na kuwa Sheria.

    Vijana hao wamewataka wabunge wote kutilia maanani mapendekezo hayo na kuangusha Mswada huo bila kuzingatia mirengo Yao ya kisiasa Kwa minajili ya wananchi.