Baadhi ya viongozi wa mashirika wapongeza hatua ya Rais Ruto na Raila

  • | Citizen TV
    875 views

    Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali wakiongozwa na mwanamazingira, Daktari Isaac Kalua Green, wamempongeza Rais William Ruto kwa uamuzi wake wa kuwashirikisha viongozi wa upinzani kujadili masuala waliyoibua. Kadhalika wamempongeza kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kukubali kujadiliana na serikali na kusitisha maandamano.