- 830 viewsDuration: 3:06Madereva wa magari ya uchukuzi pamoja na wale wa magari ya kibinafsi wanaotumia barabara ya Maralal kwenda Nyahururu, wamelalamikia kuharibika Kwa barabara hiyo. Mashimo mengi kwenye barabara hiyo yamekuwa chanzo cha ajali za mara kwa mara. Madereva hao wanataka mamlaka ya ujenzi wa barabara kuu nchini KENHA kukarabati barabara hiyo. Mwanahabari wetu Bonface Barasa anaarifu zaidi kutoka Samburu.