BBC Africa Eye: Tigray yazingirwa

  • | BBC Swahili
    2,205 views
    Eneo la Tigray nchini Ethiopia limezingirwa na vita kwa takribani miaka miwili. Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na vikosi vya Tigrayan yameahirishwa na kuna ripoti za mapigano mapya. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu mtoto mmoja kati ya watatu walio chini ya miaka mitano katika eneo hilo wana utapiamlo…lakini kiwango kamili cha mzozo wa kibinadamu bado hauko wazi. Mawasiliano yamezuiwa, na waandishi wa habari wamezuiwa kuingia katika eneo hilo. Watengenezaji filamu Charles Emptaz na Oliver Jobard walifika huko mnamo Juni na walitembelea hospitali huko Tigray ambayo inatatizika kutibu wagonjwa wake. Hussein Mohamed ana ripoti hii kwa BBC Africa Eye - na onyo, ina picha za kuhuzunisha. #bbcswahili #bbcafricaeye #ethiopia