Bibi wa miaka 80 arudi shule na kufanya mitihani yake ya darasa la 12.

  • | BBC Swahili
    355 views
    Ratnakumari Sunuwar 80, kutoka kijiji cha mbali cha wilaya ya Ramechhap mashariki mwa Nepal, hakuwahi kupata nafasi ya kwenda shule. Alikuwa mkulima akisaidia kipato nyumbani, kisha mama wa nyumbani, na baadaye, akajaaliwa watoto. Lakini baada ya watoto wake kukua, alianza kusoma tena. Alifanyia mitihani ya darasa la 12 mwezi Mei. Ratnakumari anasema hasomi ili kupata kazi, lakini kuwatia moyo vijana wanaoacha shule. #bbcswahili #india #elimu