- 128 viewsHuku wanafunzi wa gredi ya 10 wakiendelea kuripoti shule mbalimbali nchini, binti mmoja kutoka eneo la Kitutu Masaba amelazimika kuwa mjakazi, licha ya kupata nafasi katika shule ya kitaifa. Cecilia Kerubo ameshindwa kwenda katika shule ya upili ya Litein iliyoko kaunti ya Kericho alikotarajiwa kuripoti. Kerubo anasema bado hajakata tamaa kuwa ndoto yake ya kuwa Daktari itatimia