Skip to main content
Skip to main content

Bitok atoa onyo kali kwa wahusika wa ghasia shuleni

  • | Citizen TV
    436 views
    Katibu wa Wizara ya Elimu Julius Bitok ametoa onyo kali kwa wanafunzi na watu wanaohusika na ghasia pamoja na uharibifu wa mali katika shule mbalimbali nchini kwamba kila mmoja atabeba msalaba wake. Kauli yake inajiri wakati ambapo kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya utovu wa nidhamu shuleni na kusababisha baadhi ya shule kuwatuma wanafunzi nyumbani. Hata hivyo, Wizara ya Elimu imesisitiza kuwa kalenda ya masomo haitatatizika, ikisisitiza kuwa ni idadi ndogo tu ya shule ambazo zimeathiriwa na matukio hayo.