Blinken atoa msimamo juu ya usimamizi wa Gaza

  • | VOA Swahili
    450 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken Jumatano amesema Ukanda wa Gaza hauwezi kuendeshwa na Hamas au kukaliwa kimabavu na Israel baada ya vita vya karibuni katika eneo la Palestina. Blinken alisema kipindi cha mpito baada ya kumalizika kwa mzozo huenda kikawa ni muhimu hilo kusisitizwa “ ni muhimu kwamba watu wa Palestina wawe ni kiini cha utawala huko Gaza na Ukingo wa Magharibi pia, na kwamba, kwa mara nyingine, hatuoni eneo hilo kukaliwa kimabavu.” Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hakufafanua wiki hii lini alisema kwamba Israel itadhibiti kwa muda usiojulikana “majukumu yote ya ulinzi” huko Gaza mara atakapowaondoa madarakani wanamgambo wa Hamas. Lakini yaliyotokea siku zilizopita yanapendekeza kwa jukumu lolote la ulinzi la Israel litaonekana kuwa ni ukaliaji wa kimabavu, hasa na jumuiya ya kiamtaifa ambayo itaona ni aina fulani ya uvamizi wa kijeshi, na kukanganya mipango yoyote ya kukabidhi majukumu ya utawala kwa Mamlaka ya Palestina au mataifa rafiki ya kiarabu. Hata kama Israel itafanikiwa kumaliza utawala wa miaka 16 wa Hamas huko Gaza na kuvunja miundo mbinu ya wanamgambo, uwepo wa majeshi ya Israel huenda ukachochea uasi, kama ilivyotokea kutoka mwaka 1967 mpaka 2005, kipindi ambacho kulishuhudiwa kuwepo kwa uasi kwa Palestina na kuibuka kwa Hamas. #israel #gaza #iran #reels #igreels #voa #hamas #waziri #mamboyanje #antonyblinken