Bunge la Meru limepitisha makadirio ya bajeti

  • | Citizen TV
    276 views

    bunge la Kaunti ya Meru limepitisha makadirio ya bajeti ya mwaka wa 2024/25.Bajeti hiyo ya aina yake, imetengea kila mradi wa Maendeleo fedha zake, tofauti na hapo awali ambapo fedha zilikuwa zinatengewa idara kwa ujumla na kuwaachia waziri wa kaunti kuamua miradi itakayotekelezwa. Kila wadi itapata mgao wa Maendeleo wa shilingi Milioni 45.wawakilishi wadi, wamesema hatua hiyo itahakikisha Maendeleo yanafika katika kila wadi.Wakilishi wadi hao wameondoa fedha za Mradi wa Ng'ombe ambao unashabikiwa na gavana kawira mwangaza Wakisema Ngavana hakuwasilisha mswada wa kutoa mwongozo kuhusu mradi huo, na pia kuwa wananchi waliukataa wakati wa ukusanyaji wa maoni ya umma.