Chama cha ANC chaongoza kwa kura Afrika Kusini, ila wabunge wachache

  • | Citizen TV
    4,234 views

    Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Afrika Kusini huku matokeo ya awali kutoka baadhi ya maeneo ya taifa hilo yakiendelea kuonesha chama tawala cha African National Congress ANC, kinapoteza wingi wa viti bungeni. Ni matokeo ambayo vijana wengi nchini Afrika Kusini wanasema huenda ikawa ushindi kwao kama yataendelea kukiweka ANC katika nafasi ambayo kitashindwa kuunda serikali peke yake. Kutoka Pretoria, Bryson Bichwa ana taarifa