Chama cha wanahabari chalalamikia kampuni ya Standard Group kukosa kulipa wafanyikazi mishahara yao

  • | Citizen TV
    623 views

    Chama cha wanahabari nchini KUJ sasa kinatishia kufanya mgomo kulalamikia kampuni ya habari ya Standard Group kwa kutowalipa wafanyakazi wake mishahara. Kwenye kikao hapa Nairobi, chama cha KUJ kikishirikiana na mashirika mengine yanayowasimamia wanahabari wamelalamikia mahangaiko ya wafanyakazi wa kampuni ya standard group kwa kutowalipa wafanyakazi wake kwa hadi miezi 10. Sasa wanataka wasimamizi wanaodai walisababisha kusambaratika kwa shughuli katika kampuni hii kuchukuliwa hatua na kwa kampuni hiyo kuwalipa wafanyakazi wake mara moja