COTU yapinga pendekezo la ajira ya watumishi wa umma kwa kandarasi

  • | KBC Video
    37 views

    Muungano wa vyama vya wafanyakazi, COTU, umepinga mpango wa serikali wa kubadili masharti ya kudumu ya ajira ya watumishi wote wa umma kuwa ya kandarasi kama njia ya kudhibiti kiwango cha juu cha mishahara. Akizungumza wakati wa mkutano wa waakilishi wa wafanyakazi katika makao makuu ya muungano huo jijini Nairobi, katibu mkuu Francis Atwoli alisema kuwa pendekezo hilo la wizara ya utumishi wa umma litasambaratisha utumishi wa umma na pia kuathiri utenda kazi. Na jinsi mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anavyotuarifu vyama vya wafanyakazi vimeorodhesha shinikizo zinazotaka zishughulikiwe na serikali wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi tarehe mosi mwezi ujao zitakazoandaliwa katika uga wa Uhuru Gardens.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive