- 723 viewsDuration: 1:43Tofauti umeibuka ndani ya jamii ya Samawadhal inaoishi kaunti ya Garissa baada ya wale wanaoonekana kwenda kinyume na msimamo na uamuzi wa baraza la wazee ya jamii hiyo kuhusu demokrasia ya maelewano kutimuliwa. Hivi karibuni kumekuwa na mchujo wa watakaowania viti tofauti vya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao ambapo majina ya watu fulani yalipendekezwa kuwania viti hivyo lakini baadhi ya wazee katika baraza hilo walipinga na kusababisha kutimuliwa kwao. Baraza la wazee katika jamii ya wasomali lina mamlaka makuu ya kuamua atakayewania kiti cha kisiasa na kukaidi maamuzi wake lina matokeo yake.