Skip to main content
Skip to main content

Dhana potovu na ukosefu wa maadili zinachangia idadi ndogo ya wanafunzi katika vyuo vya kiufundi

  • | Citizen TV
    103 views
    Duration: 2:26
    Ukosefu wa maadili na dhana potovu ya kupokea masomo kwa miaka mitatu imetajwa kama changamoto kuu inayokumba vyuo vya ufundi kuendelea kurekodi idadi ndogo ya wanafunzi nchini. Akiongea huko mombasa katika hafla ya ufunguzi wa kongamano linalolenga kubuni mikakati ya kuhakikisha vijana wamejiunga na vyuo vya ufundi pamoja na kupokea mafunzo yanayolingana na viwanda vilivyoko nchini, katibu katika wizara ya elimu Esther Muoria amedokeza kuwa serikali imekubali kushirikiana na viwanda vya humu nchini kuwekeza ndani ya taasisi za kiufundi ili kutoa mafunzo na vifaa vinavyohitajika kwa taaluma mbali mbali.