Waziri wa ardhi, nyumba na ustawi wa miji, Alice Wahome amehakikishia wakenya kwamba mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uko kwenye mkondo unaostahili. Waziri aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya ghafla kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu huko Olkalou, kaunti ya Nyandarua. Wahome alitangaza kwamba nyumba-520 zinajengwa katika eneo hilo, huku nyumba-100 tayari zikiwa zimekamilika na asilimia 40 ya nyumba nyingine ikikaribia kukamilika.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive