Dkt. Hongo: Utundu wa wanafunzi unaashiria matatizo ya akili

  • | Citizen TV
    124 views

    Wataalamu wa afya ya akili wanasema visa vya magonjwa ya akili vinazidi kuongezeka nchini, hivyo basi kuna haja ya serikali kuwekeza raslimali ya kutosha kuimarisha afya ya akili hususan miongoni mwa walimu na wanafunzi shuleni. Akizungumza katika kongamano la taasisi za kanisa katoliki jijini nairobi, afisa mkuu katika hospitali ya Chiromo daktari vincent hongo ameeleza kwamba utundu na ghasia shuleni ni dalili za matatizo ya akili na kwamba kuna haja ya kuwasaidia wanafunzi badala ya kuwaadhibu.