DPP aagiza kushtakiwa kwa Gavana wa Bomet Barchok, Wangamati na Dan Wanyama kwa tuhuma za ufisadi

  • | Citizen TV
    764 views

    Gavana wa Bomet Hillary Barchok pamoja na mwenzake wa Zamani wa Bungoma Wycliffe Wangamati ni miongoni mwa watu walioidhinishwa kufunguliwa mashtaka na mkurugenzi wa mashtaka ya umma kwa tuhuma za ufisadi. Wengine wanaotuhumiwa kushiriki ufisadi ni pamoja na Mbunge wa Webuye West Dan Wanyama. Hatua ya mkurugenzi wa mashtaka ikijiri baada ya Tume ya Maadili na kupambana na ufisadi EACC kuwasilisha ushahidi wiki jana.