Duka la uuzaji simu zilizoibwa lafumaniwa Nairobi

  • | KBC Video
    8,026 views

    Katika juhudi za kukabiliana na visa vya wizi wa simu hasa jijini Nairobi, polisi wamefumania msako katika duka moja linalouza simu za wizi katika barabara ya Munyu na Mfangano, na kuwakamata washukiwa sita. Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi George Seda, simu za thamani ya shilingi milioni tatu na zaidi ya shilingi laki sita pesa taslimu zilipatikana katika oparesheni hiyo. Kamanda huyo sasa amewahimiza wale waliopoteza simu zao ama vifaa vyao vya elekroniki kufika katika kituo cha polisi cha Central, ili kutambua vifaa vyao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive