Tume ya kupambana na ufisadi EACC imeanzisha uchunguzi ya madai ya unyakuzi wa ardhi ya umma katika eneo la Kasagam kaunti ya Kisumu. Mkurugenzi wa EACC eneo la Nyanza Abraham Kemboi amesema kuwa kipande hicho kinachopakana na kituo cha polisi cha Kasagam, kinapaniwa kutumika kwa ujenzi wa makao ya maafisa wa polisi. Kaunti ya Kisumu ilitajwa kama moja ya kaunti zenye visa vingi vya unyakuzi wa ardhi ya umma, ambapo mwaka jana, tume hiyo ilirejesha ardhi yenye thamani ya shilingi milioni mia tatu kwa asasi za serikali .