EACC yaikabidhi serikali ardhi ya shilingi bilioni 5

  • | Citizen TV
    695 views

    Tume ya kupambana na ufisadi nchinI EACC imeikabidhi serikali ardhi ya thamani ya shilingi bilioni tano na mali nyingine za umma zilizokuwa zimetwaliwa kwa njia za ufisadi. Rais Ruto amepokezwa sajili ya mali hizi huku akisema kuwa hatatia saini mabadiliko ya mswada wa mkinzano wa maslahi utakaowaruhusu maafisa wa serikali pamoja na familia zao kupata zabuni za serikali.