Eugene Wamalwa asema Azimio itasalia imara licha ya Raila Odinga kuwania uwenyekiti AU

  • | Citizen TV
    490 views

    Kiongozi wa Chama cha DAP-K Eugene Wamalwa amesema kuwa Azimio itasalia imara licha ya azma ya kinara wake Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa umoja wa Afrika. Akihutubia waumini katika hafla ya kanisa la ACK Chebuyusi eneo bunge la Lurambi, Wamalwa aliwapongeza wanasiasa wa mrengo wa Kenya Kwanza kwa kuunga mkono azma ya Raila Odinga.